MARIETHA MZIMU UNAOISHI

Marietha,mzimu unaoishi.
sehemu:1
Mwandishi: Agatha Francis

"karibu sana dada yangu, karibu,ilikua sauti ya msichana akimkaribisha aliyemuita dada Kwa furaha huku akimkumbatia."Asante sana mdogo wangu",yule dada pia alijibu kwa kufurahi Sana. Kisha yule dada alimkaribisha ndani Kwa furaha na mgeni pia alikaribia ndani bila shaka Lolote.
   Walipofika Ndani,alimkaribisha katika moja ya sofa zilizokuwepo mule Ndani,kisha alikwenda katika friji nakutoa soda moja nakumpatia mgeni wake. Alipokua anainywa soda ile yule dada mwenyeji aliuliza hali ya mama nyumbani,pasipo shida yoyote mgeni yule pia alieleza kua nyumbani wazima wa afya ila wamemkumbuka sana yeye ambaye kwasasa yupo mbali,basi walicheka sana kwani aliamini kwakukumbukwa kumbe nayeye alipendwa kisha yule dada mgeni alihoji "vipi shemeji yupo?", dada mwenyeji alijibu "hapana kaenda kazini lakini muda si mrefu atarudi maana hii ndiyo mida yake"basi dada mwenyeji aliinuka nakuingia jikoni kuandaa chakula.
  Sebuleni alibaki dada mgeni peke yake akiendelea kuangalia runinga iliyokuwepo sebuleni pale, alipokua akiendelea fanya hivyo shemeji yake aliingia. Alikua kijana mdogo mdogo aliyeendana na mke wake, alipoingia tu alishangaa kumuona shemeji yake akasema "ooh shemeji kimya kimya tena sio vizuri hivyo",alisema huku akitabasamu,shemeji yake alitabasamu kisha akasema"nimeamua kuwasuprise leo kwani vibaya",alisema hayo huku akiinuka kumsalimia shemeji yake.
Je nini kitafuata katika hadithi hii yakusisimua......... ITAENDELEA BAADAE [SHARE ]                                          ðŸ˜€ðŸ˜€ðŸ˜€ kwa simulizi zaidi gusa hapa www.Facebook.com/storizakitaa2015

        BY ___ALEX MUSSA___

Comments