MARIETHA MZIMU UNAOISHI

Marieth
a,mzimu unaoishi.
Sehemu ya 2
Mwandishi: Agatha Francis

"hapana sio vibaya shemeji yang, na nimefurahi Sana kukuona hapa kwetu leo",alipoongea maneno hayo kwa tabasamu nono sana lililojidhihirisha usoni kwake alimuuliza tena shemeji yake huku wote wawili wakiketi chini"mke wangu mariamu yuko wapi?nakuona umebaki Peke yako hapa, alizungumza huku akicheka.Shemeji ambaye ni yule dada mgeni alijibu kwa kutabasamu "yupo jikoni, usiniambie umemkumbuka Tayari,kisha alicheka."ndiyo nimemkumbuka siunajua tena yule ni daktari wangu mdogo mdogo,aliposema hivyo wote wawili walicheka Sana tena sana wawili hawa walionesha kufahamiana kiasi mpaka wakajikuta wamezoeana Sana.Basi sebuleni palienea vicheko tu hali iliyomfanya aliyekuwepo jikoni kushtushwa na cheko zile, yaani Dada ambaye sasa tumejua jina lake baada ya mumewe kuuliza alipo,anaitwa Mariamu.Mariamu kimuonekano ni binti ambaye ukimtazama utapenda alivyo, ni binti mpole,si muongeaji na mwenye upendo sana kwa walio karibu yake na haswa mume wake.Lakini ni binti ambaye ukimtazama vizuri utagundua anamatatizo sana katika kichwa chake kwani tangu kuolewa na mume wake hakupenda kujichanganya alikua ni yeye na mume wake,mume hayupo ni yeye na ndani kwake richa ya uzuri wake wa sura na tabia hakua na rafiki hata jirani yake zaidi ya dada yake huyo aliyefika hapo,majirani walimsema wajuavyo kuna waliosema anaringa kisa mme wake mwalimu vimshahara vinamsumbua subiri apauke,wengine walisema itakua mchawi huyo kwanini asiongee na wengine..ITAENDELEA Usikose 3 SHARE


       BY ____ALEX MUSSA____

Comments