Waziri mkuu azungumza kuhusu vyuo vifivyofungiwa Udahili

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, amevitaka vyuo vikuu vilivyofungiwa kudahili wanafunzi kwa mwaka wa masomo 2017/2018 amevitaka kukamilisha matakwa yanayohitajika na kufuata taratibu zilizowekwa na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU).
Hayo yameelezwa na Waziri Majaliwa, wakati wa ufunguzi wa maonesho ya 12 ya vyuo vikuu nchini yanayofanyika viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini, Dar es Salaam.
“Vyuo vikuu vyote nchini vinatakiwa kutoa elimu bora kwa wahitimu ili kuwawezesha kujiajiri na kuendana na Sera ya Serikali ya awamu ya tano ya kujenga Tanzania yenye viwanda,” amesema Majaliwa.
Majaliwa ameongeza kuwa, ili kujenga uchumi wa viwanda vyuo vikuu hapa nchini
vinatakiwa kufundisha na kuwawezesha wahitimu kujiajiri ili kuendana na ushindani katika soko la ajira kitaifa, kimataifa na Dunia kwa ujumla.
Waziri Majaliwa alisema vile vile vinatakiwa kukuza stadi katika sekta ya viwanda kwa kupata wasomi waliofundishwa kwa vitendo kutoka katika vyuo mbalimbali, kuweka mikakati na kuboresha elimu ili kuendana na dhamira ya Serikali pamoja na kuweka mitaala mizuri kwa wanafunzi katika vyuo hivyo ili kuendana na mabadiliko yaliyofanywa katika udahili wa wanafunzi kwa mwaka wa masomo 2017/2018.

Comments