Baada ya Baraza Kuu la Uongozi la Taifa la Chama cha Wananchi (CUF) kutuma tarifa kwa Spika wa Bunge ya kuwavua uanachama wabunge 8 wa chama hicho kwa madai ya utovu wa nidhamu, Bunge limeridhia hatua hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Bunge hilo inasema
“Kufuatia barua aliyopokea Spika wa Bunge Mhe. Job Yustino Ndugai kutoka kwa Mwenyekiti Prof. Ibrahim Haruna Lipumba na Kaimu Katibu Mkuu Mhe. Magdalena Hamisi Sakaya (Mb) wa Chama cha Wananchi (CUF), Mheshimiwa Spika angependa kuwaarifu Watanzania wote kwamba amejiridhisha kuwa Wabunge hao wamefukuzwa Uanachama kulingana na taratibu za Chama hicho na hivyo wamekosa sifa za kuendelea na Ubunge.
Wabunge hao ni: – Mhe. Severina Silvanus Mwijage, (MB); Mhe. Saumu Heri Sakala, (MB); Mhe. Salma Mohamed Mwassa, (MB); Mhe. Riziki Shahari Mngwali, (MB); Mhe. Raisa Abdallah Mussa, (MB); Mhe. Miza Bakari Haji, (MB); Mhe. Hadija Salum Ally Al-Qassmy, (MB); na Mhe. Halima Ali Mohamed, (MB).
Hivyo, kwa mamlaka aliyonayo kwa kuzingatia kifungu cha 67(1)(b) cha Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 kikisomwa pamoja na kifungu 37(3) cha Sheria ya Uchaguzi Sura 343 kama ilivyojadidiwa Mwaka 2015, Mheshimiwa Spika ametangaza nafasi hizo kuwa wazi na pia kumuandikia Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ili aendelee na hatua zinazostahili kujaza nafasi hizo kwa Mujibu wa Sheria na Taratibu zilizopo,”.

Comments
Post a Comment