Mwanaume mmoja mkazi wa Sumbawanga Amuua mkewe kwa kumchoma na kisu

Mtu mmoja ameuwawa kwa kuchomwa kisu katika kata ya mafulala manispaa ya sumbawanga mkoani rukwa kwa jina anna kasha magula (mama gulo) na mume wake kwa kile kilicho onesha kuwa ni mgongano wa maneno,nae mwenyekiti wa mtaa kata ya mafulala christopha kalingi alieleza kuwa kilicho sababisha kifo hicho mtuhumiwa aliulizwa na mkewe pesa alizo mpatia shilingi elfu thelathini amezifanyia nini ndipo hapo mtuhumiwa alipo anza kutoa vitisho vingi kwa mkewe na kupelekea kumchoma kisu mkewe na kusababisha kifo, nae mtoto wa marehemu aliezea mkasa huo kwa majonzi mazito mkasa huo ulitokea mida ya saa sita usiku na kuweza kutimiza adhima yake na kisha kukimbia huku akiwa amewafungia watoto wake kwa nje ,jeshi la police liliweza kufika katika eneo la tukio katika midaa ya saa nane usiku na kupata maelezo kutoka kwa wananchi walio shuhudia tukio hilo, nao wananchi waliweza kutoa maoni yao kwa jeshi la police kuweza kufika kwa wakati katika maeneo ya matukio, pamoja na hayo sala mwangale shuhuda wa tukio hilo aliweza kutoa ushauri wake kwa wababa waweze kujilekebisha kwani mama ndiye msingi wa familia
    
        BY ALEX MUSSA

Comments