MGANGA MFAWIDHI ASIMAMISHWA KAZI BAADA KUKIUKA AGIZO LA SERIKALI.

Baada ya serikali kupitia Waziri wa Afya, Jinsia ,Wazee na Watoto, kupiga marufuku mama mjamzito, mtoto chini ya miaka mitano na mzee wanapata huduma bure. Waziri Ummy Mwalimu ,amemsimamisha kazi mganga mfawidhi wa kituo cha afya Mlandizi, Dkt. Mpola Tamambele,kutokana na kushindwa kusimamia maelekezo hayo.
Kusimamishwa kazi kwa Mfawidhi huyo kuna kuja baada ya Kutokana na mama aliyejifungua, Bi Salma Khalifan kwenda kununua vifaa vya kujifungulia vya sh.180,000 ili apate huduma .
Kutokuwa na mamlaka ya moja kwa moja amemuagiza kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya halmashauri ya wilaya ya Kibaha ,Beda Mmbaga kumsimamisha kazi mganga mfawidhi huyo mara moja wakati uchunguzi wa tuhuma zinazomkabili zikiendelea .
Waziri Ummy liyasema hayo wakati alipokwenda kutembelea kituo cha afya Mlandizi ,kabla ya kukabidhiwa kwa magari ya wagonjwa matatu kutoka kwa mbunge wa jimbo hilo ,Hamoud Jumaa.
“Sitokubali mtumishi anakwenda kinyume na serikali ,rais wetu John Magufuli anasisimamia suala zima la kuboresha huduma za afya ,halafu akitokea mtu mmoja mzembe anatuchanganya kwakweli sitoweza kumfumbia macho “
“Wananchi wamekuwa waoga hata kuingia katika suala la bima ya afya kwa sababu ya mambo kama haya ,namsimamisha mganga mfawidhi huyo hadi hapo uchunguzi utakapokamilika .” alisema Ummy .
Aidha Waziri huyo alisema yeye hana mamlaka ya moja kwa moja kumsimamisha kazi mganga mfawidhi huyo hivyo anaiachia mamlaka husika isimamie jukumu hilo.

Comments