Kimenuka Baraka Da Prince amuita Alikiba mpuuzi soma hapa

Msanii Baraka da prince ambaye wiki iliyopita alitangaza rasmi kujitoa kwenye lebo ya Rock star ambayo Ali kiba ni moja kati ya wamiliki wa lebo hiyo leo akiwa kwenye kipindi cha The base cha Itv akitambulisha ngoma mpya ya msanii kutoka kwenye lebo yake ya Bana Music amemjibu Ali kiba kwa kumuita mpuuzi.

Baraka aliyajibu hayo baada ya kuulizwa kuhusu kauli ya Ali kiba kusema kuwa Baraka ana akili za kitoto “Hiyo ni kauli ya kipuuzi so siwezi kufatilia mambo ya kipuuzi na yeyote atakaye ongea kauli hiyo ya kipuuzi ni mpuuzi” ilikuwa kauli ya Baraka ambayo ilimlenga wazi Ali kiba kwa kuwa yeye ndio aliyesema kuwa Baraka ana akili za kitoto.

Lakini mbali na hivyo bado Baraka amekanusha kuwa na tatizo na uongozi wake wa awali na yuko tayari kufanya kazi na uongozi huo ila hayupo tayari kusimamiwa tena na uongozi huo pia amekiri kuwa yeye ndio alikuwa amevunja mkataba.Kwa sasa Baraka anajisimamia mwenyewe chini ya lebo yake ya Bana pamoja na mpenzi wake Naj ambaye ameachia ngoma yake mpya iitwayo Utanielewa.
.
.
TOA MAONI YAKO HAPA

Comments